Enock Maregesi quotes:

+1
Share
Pin
Like
Send
Share
  • Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Tanzania alikuwa mlezi; wa ndoto ya haki, amani, uzalendo, ujamaa, na uhuru.

  • Baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi katika bustani ya Edeni, kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Kwa hiyo dhambi hutokana na maisha, na maisha hutokana na dhambi.

  • Serikali inayodhulumu wananchi wake ni hatari kuliko simba.

  • Mandela alikuwa hodari ndiyo maana akapelekwa jela. Alikuwa mvumilivu ndiyo maana akakaa jela kwa miaka ishirini na saba. Alivyotoka akawa kiongozi bora wa Afrika Kusini. Utu ukafanya awasamehe binadamu wenzake. Urithi wa Nelson Mandela kwetu ni uhodari, uvumilivu, uongozi bora, utu na msamaha kwa binadamu wenzetu. Mandela alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Afrika Kusini alikuwa mlezi wa ndoto, ya amani na uhuru.

  • Acha alama katika dunia baada ya kuondoka.

  • Tunazaliwa na kufa. Lakini hatujui tunakotoka. Wala hatujui tunakokwenda. Huenda tunatoka na kwenda katika dunia nyingine, ya ulimwengu mwingine, hivyo kutufanya wageni wa dunia yetu wenyewe. Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta.

  • Ni rahisi kushinda vita ya maisha na kuishi mbinguni duniani. Ni vigumu kushinda vita ya dhambi na kuishi mbinguni paradiso.

  • Kutunza siri wakati mwingine ni kitu kigumu sana kwa baadhi ya watu lakini watu wanapaswa kuwa na uwezo wa kutunza siri kujijengea uaminifu, ambao ni siri ya mafanikio.

  • Kitabu cha KOLONIA SANTITA kinaweza kusomwa na watu wenye umri wa kuanzia miaka 13 na kuendelea. Katika umri wa miaka 13 fikra za mtoto huanza kuwa na maono na utambuzi wa vitu mbalimbali. Watoto katika umri huu wanao uwezo wa kuchambua dhana kadha wa kadha za kinadharia, na hali kadhalika wanao uwezo wa kuchambua nadharia tata zisizokuwa na uhakika, kama nadharia ya KOLONIA SANTITA.

  • Maisha ni kani au 'force' ya kipekee zaidi katika ulimwengu unaofahamika; achilia mbali changamani ('complexity') na kutapakaa ('diversity') zaidi kuliko kani zote! Ni tukio la ajabu kuliko matukio yote yaliyowahi kutokea.

  • Maisha ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni.

  • Maskini hana nidhamu ya mapato na matumizi. Tajiri ana nidhamu ya mapato na matumizi.

  • Fikiri kama anavyofikiri tajiri. Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.

  • Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo.

  • Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine.

  • Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake. Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake.

  • Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya. Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri.

  • Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi.

  • Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake.

  • Kuna vita za aina mbili zinazopiganwa hapa duniani: vita ya maisha na vita ya dhambi. Unaweza kushinda vita ya maisha (maisha ya raha) lakini ukashindwa vita ya dhambi (maisha ya laana). Kushinda vita ya dhambi ni lazima umkaribishe Mwana wa Mungu Mfalme wa Amani, Yesu Kristo wa Nazareti Aliye Hai, kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

  • Dunia ni uwanja wa vita wa vita ya dhambi ya vita ya maisha! Kuishi maisha ya kufikirika ni kushinda vita ya maisha ya vita ya dhambi. Vita ya dhambi ya vita ya maisha si vita ya kufikirika! Bila Yesu katika maisha yetu hakuna atakayeishinda.

  • Vita ya dhambi hupiganwa katika uwanja wa akili na katika uwanja wa mwili kati ya Shetani na Mungu. Hutumia silaha kuu ya uongo na silaha kuu ya ukweli. Mungu anataka tuujue ukweli. Shetani anataka tuujue uongo. Kushinda vita ya dhambi huna budi kutumia neno la Mungu, kama Yesu alivyolitumia kumshinda Shetani wakati akijaribiwa katika Mlima wa Majaribu wa Jangwa la Yuda.

  • Hadithi ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema hadithi yangu si ya kweli?

  • Kuandika hadithi ni kitu kimoja. Kuweka kanuni za fasihi katika hadithi ni kitu kingine.

  • Kanuni za fasihi ndiyo msingi wa maandiko yote ya kitaalamu hapa ulimwenguni. Watu hawana budi kuzifuata kanuni hizo kama wanataka kutumia vipaji vyao katika ngazi ya kimataifa.

  • Nini kingetokea kama Adamu na Hawa wasingekula tunda la Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya mpaka siku ya Sabato? Mungu angewaruhusu kula na lengo la uumbaji wa Mungu lingekamilika. Wanadamu wakifuata Amri Kumi za Mungu katika maisha yao watakuwa na uwezo maalumu ambao baadaye utawawezesha, kupitia Roho Mtakatifu, kuwa na maarifa ya siri ya uumbaji wa Mungu.

  • Mungu akikuweka mahali unapostahili kuwa, kulingana na takdiri ya maisha yako, hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindana na kipaji chako.

  • Zaka husaidia kueneza injili duniani kote. Ukitoa zaka umesaidia kueneza injili duniani kote. Toa zaka na mapato yako yatabarikiwa. Usitoe zaka na mapato yako yatalaaniwa.

  • Ukitaka kujua vipaji vyako ulivyopewa na Mungu mtumikie Mungu katika kitu fulani kwa nguvu zako zote.

  • Kuzaliwa na kuishi ni mibaraka mikubwa ya Mwenyezi Mungu kuliko yote duniani.

  • Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda. Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda.

  • Maskini hudhani kuwa tajiri lazima usome sana. Tajiri hudhani kuwa tajiri si lazima usome sana.

  • Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita. Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja.

  • Maskini huamini ili uwe tajiri lazima ufanye kitu fulani. Tajiri huamini ili uwe tajiri lazima uwe kitu fulani.

  • Maskini hupenda kuburudishwa kuliko kuelimishwa. Tajiri hupenda kuelimishwa kuliko kuburudishwa.

  • Maskini ana woga. Tajiri hana woga.

  • Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri.

  • Kama una akili kuwa kawaida. Kama una nguvu kuwa mkarimu. Kama una pesa kuwa mnyenyekevu. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa na pesa kuwa mnyenyekevu.

  • If you are smart be simple. If you are powerful be generous. If you are rich be humble. If you want to be smart be simple. If you want to be powerful be generous. If you want to be rich be humble.

  • Maskini mwenye pesa nyingi ni tajiri bahili. Tajiri mwenye mifuko iliyotoboka ni tajiri badhiri.

  • Toa msaada katika jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo.

  • Heri kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka, kuliko kusema mbele za watu kwamba pesa haijakupa furaha. Wengi hupata jeuri ya kusema hivyo kutokana na umaskini wa watu wanaowazunguka.

  • Mtu anayesema pesa haijampa furaha hana nia ya kusaidia watu.

  • Kuwa tajiri si kazi rahisi. Ukipata milioni ya kwanza utataka nyingine kulinda hiyo ya kwanza. Ukipata ya pili utataka mbili zingine kulinda hizo mbili za kwanza, n.k. Si kazi rahisi. Si kama unavyofikiria. Utajiri haujanipa furaha. Umenipa uhuru. Ndugu zangu ni maskini wa kutupwa. Ningependa kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi.

  • Ukarimu ni bora kuliko hekima, na kulitambua hilo ndiyo mwanzo wa hekima.

  • Sentensi ni mkusanyiko wa maneno unaoanza na herufi kubwa na kuisha na alama ya kushangaa, kuuliza, au nukta. Sentensi bora ni fupi, angavu, sahihi, yenye mantiki, na kamilifu.

  • Sentensi bora katika medani ya uandishi ni sentensi fupi, angavu, sahihi, yenye mantiki, na kamilifu.

  • Usiwapoteze marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wako, wala usiwaache marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wao.

  • Marafiki zako wa mwanzo ni wazuri kuliko wote.

  • Maskini hajali wewe ni nani. Anajali utu ndani ya moyo wako.

  • Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa. Tajiri hutumia pesa kupata pesa.

  • Kwa mwanamke wa kuoa natafuta hasanati. Akiwa mbaya atakuwa mzuri. Akiwa maskini atakuwa tajiri. Akiwa gumbaru atakuwa msomi. Akiwa mshamba atakuwa mjanja. Akiwa mjinga atapata maarifa. Nitampenda zaidi kwa mazuri kuliko mabaya.

  • Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa kadiri unavyozidi kujitolea kwa ajili ya watu wengine ndivyo unavyozidi kuwa maskini, lakini hii si kweli. Huduma kwa ajili ya watu wengine huleta maana fulani na ukamilifu katika maisha yetu kwa namna ambayo utajiri, madaraka na mali haviwezi kushindana nao. Mungu hababaishwi na kiasi gani unatoa. Anababaishwa na imani uliyonayo wakati unatoa. Ukitoa kidogo inatosha. Ukitoa kingi inatosha pia.

  • No matter how talented or skilled you are, you will never reach your full potential without expert guidance.

  • Kujitolea kwa moyo mmoja kwa muda mrefu huleta furaha na afya njema kwa mtoaji na kwa mpokeaji pia.

  • Kutakuwepo na nguvu za chanya na hasi katika maisha yako kadiri utakavyoishi hapa duniani. Ukiruhusu moyo wako kuwa chanya utakuwa chanya. Ukiruhusu moyo wako kuwa hasi utakuwa hasi. Shetani hawezi kuona ndani ya moyo wako mpaka wewe mwenyewe umwonyeshe. Ukionyesha chanya Mungu atakupa chanya. Ukionyesha hasi Shetani atakupa hasi.

  • Kila mmoja wetu ana kitu cha kutoa. Wengine wana pesa, wengine wana vipaji, wengine wana muda. Vipaji vyote tulivyopewa na Mungu, vikubwa au vidogo, hatuna budi kuvitumia kiukarimu kwa watu wanaovihitaji. Tunapofanya hivyo tunaleta mabadiliko katika dunia kwa ajili ya watu fulani, na tunapata maana halisi ya maisha na toshelezo la moyo katika maisha yetu.

  • Vichwa vitatu vya sururu na chembe tatu za bunduki za Kalashnikov; na alama ya bahati, mafanikio, udhalimu na mwanzo mpya ya msalaba wa swastika, kama alama ya ujenzi na uhalifu wa Kolonia Santita.

  • Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi.

  • Serikali mara nyingi hutegemea ujasusi wa ndani na nje kufanya maamuzi mazito na sahihi ya kuendesha nchi.

  • Wananchi wataendelea kuwepo hata kama serikali haitakuwepo. Serikali haiwezi kuwashinda wananchi. Sauti ya umma ni sauti ya Mungu. Serikali haiwezi kumshinda Mungu.

  • Wananchi wakiamua kufanya kitu katika nchi yao kwa asilimia 100 serikali, na taasisi zake zote, haitaweza kuwazuia. Kwa sababu, mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali.

  • Kushirikiana na maadui wa nchi yetu ni hatia ya kosa la uhaini. Adhabu yake ni kifo, au kifungo cha maisha.

  • Kati ya nchi yako na serikali yako ni kitu gani unakipenda zaidi? Ipende zaidi nchi yako, kuliko serikali yako!

  • Unaweza kusaliti nchi kwa sababu za kiitikadi, kisiasa, matatizo ya akili, au pesa. Ukifanya hivyo na ukabainika; utawajibika kwa adhabu ya kifo, au maisha.

  • Ukiipenda sana nchi yako ni rahisi sana kuichukia serikali yake!

  • Kusaliti nchi, ambayo majeshi ya ulinzi na usalama yameundwa kuilinda, ni miongoni mwa makosa makubwa kabisa kuweza kufanywa na mtu! Adhabu yake ni kifungo cha maisha jela, au kunyongwa hadi kufa.

  • Serikali imepewa mamlaka na wananchi kuwaendeshea nchi yao. Mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali.

  • Ukifanya maamuzi kubaliana na matatizo yake.

  • Mimi ni mwana wa Mungu. Sisi sote ni watoto wa Mungu. Lengo la kuzaliwa kwangu ni kufanya kazi pamoja na Roho Mtakatifu na malaika kumtumikia Bwana, na kueneza injili ya Yesu Kristo duniani kote, kupitia vitabu.

  • Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa.

  • Kitabu cha 'Kolonia Santita' ni kitabu cha wasomi na wasiokuwa wasomi, watu wa mijini na watu wa vijijini, watu wazima, vijana na watoto. Hadhira ya kitabu hiki ni jamii nzima ya Tanzania.

  • Ukiwanyima watoto uhuru wa kuwa watoto leo watakuwa na uhuru wa kuwa watoto kesho.

  • Wakati mwingine tukitaka kutambulika hatuna budi kuweka mbele aibu ya heshima yetu.

  • People don't follow ordinary people; they follow extraordinary people.

  • Tunasema uongo kwa sababu hatuna ujasiri wa kusema ukweli. Ukweli hautupi uhuru, unatupa upweke.

  • Sina nyemi na mwanamke mwenye sura nzuri na tabia mbaya. Nina nyemi na mwanamke mwenye sura mbaya na tabia nzuri, au mwanamke mwenye sura nzuri na tabia nzuri. Mwanamke wa kuoa sitampenda nitampendelea.

  • Mwanamke akikuomba pesa, mpe!

  • Kama unataka kuijua vizuri historia ya mwanamke hasa mwanamke unayetaka kuoana naye, usifanye naye mapenzi kwa miezi sita angalau. Ukifanya naye mapenzi kwa miezi sita au zaidi, au ndani ya miezi sita, halafu akakuchanganya kimapenzi, hutakuwa na uwezo mkubwa wa kuwasikiliza watu kuhusiana na historia yake.

  • Mwaka mmoja na nusu unatosha kumjua mwanamke kabla ya ndoa. Miezi sita itakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mchumba. Mwaka mmoja na nusu utakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mke.

  • Ukitaka kumjua mwanamke jua historia yake.

  • Ukikosana na mwanamke usimpige mchana. Mpige usiku. Ukimpiga mchana watu watasema umemwonea. Ukimpiga usiku watu watasema huenda alikuwa na makosa. Wanawake hawatakiwi kupigwa.

  • Mtu akikutukana mwambie asante au samahani. Asante au samahani vina nguvu kuliko kuomba (asikutukane) au kutukana.

  • Mtu akikutukana mwambie asante. Akikupiga mwambie asante. Akiendelea kukupiga, pigana.

  • Maombi yako yasipojibiwa usikate tamaa, Mungu alishakusikia na tayari alishaandaa malaika wa kukuletea jibu. Jibu wakati mwingine huchelewa kufika kwa sababu ya nguvu za giza. Usiwe na haraka, muda wako ukifika utajibiwa.

  • Radia hakuwa na makosa. Wengi huishi maisha yao bure. Yeye aliishi ya kwake kwa ajili ya watu. Hakuishi tu kama raia wa Tunisia. Aliishi kama raia wa uanadamu, maadili mema na uchapakazi. Watu walimsifu kwa kuwa na kaulimbiu ya 'Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta'.

  • Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa waamini. Wanajijua vizuri zaidi, kuliko unavyowajua.

  • Mungu alisema tupendane katika shida na raha; Luka 6:27-36. Katika matatizo mpende hasimuyo. Maumivu ya watu hufanana.

  • Maumivu ya matatizo ya yule aliyekukosea hayana tofauti na maumivu ya matatizo ya wewe uliyekosewa. Adui yako (kwa mfano) akifiwa na mke aliyempenda sana, atajisikia vibaya kama utakavyojisikia vibaya kufiwa na mke uliyempenda sana. Kuwa na huruma kwa waliokukosea, wakati wa shida.

  • Kupata maarifa kutokana na shida ni jambo la kawaida maana shida ni kipimo cha akili, lakini kupata maarifa bila shida ni hekima maana hekima ni ufunguo wa maamuzi mema na udadisi wa kiakili.

  • Kupata maarifa kutokana na shida ni jambo la kawaida, lakini kupata maarifa bila shida ni hekima.

  • Waandishi ni wadadisi.

  • Waandishi wanapaswa kuwa wadadisi, kama paka, ijapokuwa udadisi ni hatari.

  • Udadisi ni hatari. Fikiri kabla ya kutenda.

  • Nina matatizo ya kiafya: Udadisi wa hali ya juu wa kiakili.

  • Udadisi ni kiboko cha ujinga.

  • Usitukane kamwe. Pigana itakapobidi.

  • Ijapokuwa maombi ya sifa yana nguvu kuliko maombi ya kushukuru, kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba.

  • Tumaini ni injini ya imani.

  • Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya mtu baada ya mtu kufariki? Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya pumzi katika kipindi ambacho mtu hana uwezo tena wa kuvuta hewa? Nini thamani ya pumzi? Thamani ya pumzi ni kukufanya uwe wewe na si udongo.

  • Mwaka mpya ukifika watu husherehekea kwa vifijo na nderemo! Pumzi ikifika hawasherehekei. Kwa nini?

  • Kwa nini tuseme a.k.a na si k.k.k au k.n.k au k.a.k? Lazima tujifunze kuipenda na kuitetea lugha yetu kwa usumbufu wa vizazi vijavyo.

  • Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. 2 + 2 = 5. Umoja una sisi, si mimi. Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano, watakuwa na nguvu ya watu watano, watakuwa na nguvu ya ziada.

  • Ndoto yako haitakufa mpaka utakapokufa. Usikate tamaa, kabisa!

  • Mtu yoyote anayedanganya ni Shetani, kwani Shetani ni baba wa uongo. Tusikubali kudanganywa ovyo, hasa watoto wetu, katika kipindi hiki cha utandawazi na teknolojia.

  • Mdanganyifu hudanganya wanaopenda kudanganywa.

  • Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu.

  • Gari ya Debbie huchukua sekunde 12 kutoka kilometa 0 mpaka kilometa 210 kwa saa. Huchukua sekunde 10 kutoka kilometa 210 kwa saa mpaka kilometa 0. Ina uwezo wa kusimama haraka kuliko inavyoweza kukimbia.

  • Watu hubariki wenzao ambao ni wakarimu, na hulaani wenzao ambao ni wabahili. Ukiwa mkarimu kwa watu umekopa neema kutoka kwa Mungu, na Mungu atakulipa kutokana na matendo yako.

  • Tunapaswa kujisikia furaha kuu tunapokumbana na majaribu mbalimbali katika maisha yetu, tukijua kwamba kujaribiwa kwa imani yetu hutufanya wavumilivu na wapiganaji katika Jina la Yesu, na tunapaswa kuruhusu uvumilivu katika maisha yetu kwa sababu Mungu hutumia uvumilivu huo kutukomaza na kutukamilisha.

  • Utakapofika mwisho wa njia, geuka. Huo ndiyo mwanzo wa njia nyingine.

  • Kigumu kuliko vyote ni kizuri kuliko vyote.

  • Ndani ya sekunde moja baada ya ulimwengu wetu kuumbwa, miaka bilioni kumi na tatu nukta saba tano iliyopita, chembe zote ndogo zinazopatikana ndani ya atomu zilitengenezwa. Zote hizo zimeshapatikana isipokuwa 'Higgs Boson', na 'Higgs Boson' ndiyo ya muhimu kuliko zote.

  • Nimewapa watoto wangu kila kitu katika maisha isipokuwa umaskini. Lakini bado wamenishinda.

  • Wape watoto wako urithi wa kutosha ili waweze kufanya kitu, lakini si urithi wa kutosha ili wasiweze kufanya kitu. Wape watoto uhuru wanaostahili kupata, uhuru wa mahesabu, lakini si uhuru wa kila kitu.

  • Ukiwapa watoto wako uhuru wa shaghalabaghala au uhuru wa kila kitu watajisahau! Wape uhuru wa mahesabu.

  • Mwachie mwanao urithi wa kutosha ili aweze kufanya kitu, lakini si urithi wa kutosha ili asiweze kufanya kitu.

  • Uko wapi ubinadamu wa watu?

  • Kama huwezi kumpenda mtu usimchukie.

  • Kukiuka Amri Kumi za Mungu si dhambi ni matawi ya dhambi. Dhambi ni kumkana Mungu na kumkubali Shetani.

+1
Share
Pin
Like
Send
Share